ULIMWENGU

  • HOME
Home → Mapenzi → FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI (TENDO LA NDOA)

FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI (TENDO LA NDOA)

Unknown
Add Comment
Mapenzi
Tuesday, August 19, 2014
                                                
    1:Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo
Wanawake ambao hufika kilele angalau mara mbili kwa wiki kila wanapo jamiiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiiana. Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.

2:Huongeza ukakamavu wa mifupa: 
Wanawake waliokoma kupata hedhi ambao pia hujamiiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis.


3:Hupunguza msongo wa mawazo:
Kujamiiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika, muscle relaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiiana. Watu wanaojamiiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu wanaojamiiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vya prostaglandins katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema.


4:Hupunguza maumivu:
Kufikia kilele wakati wa kujamiiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post menopausal syndrome symptom).


5:Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume: 
Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.


6:Huongeza uwezo wa kunusa: 
Baada ya kujamiiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa na kutambua harufu.


7Hupunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema: 
Kujamiiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. kujamiiana huchoma karibu 200 calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi.

8:Huongeza kinga ya mwili:
Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.
Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke: Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa.


9:Hudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida:
Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa.


10:Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini:
Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiiana huongeza kujiamini.

11:Huongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga:
na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke na hivyo kumwepusha na maambukizi katika njia cha mkojo.


12:Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini: 
Unapojamiiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.


13:Huongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako:
Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote.


14:Husaidia kuishi kwa muda mrefu:
Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele. DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.

15:Kujamiiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi:
Hii hutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin, ambayo huleta mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.


16:Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba:
Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku nne 


NB : Jambo kubwa la kuzingatia nikuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa 

Share this article :
Tweet
✚

Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

ZILIZOBAMBA TOP 10 NI . . .

  • LAANA:HUKU SASA NI KUTIANA NYEGE TU NA SI KITU KINGINE
    Mtazame mrembo huyu ambaye ameamua kujiingiza katika matangazo ya nguo katika moja ya duka kubwa la nguo hapa mjini(Mwenge) Kwa muj...
  • JINSI YA KUMRIDHISHA MWANAMKE KIMAPENZI
    Mambo matano (5) anayohitaji Mwanamke kutoka kwa Mwanaume Wanaume  hatimaye   kutambua kwamba  hawapo  peke yao  kitandani   na  ...
  • MWANAFUNZI AGAWA PENZI BAADA YA KUDANGANYWA KUWA ATAPELEKWA ULAYA
                                                                              Masikini huyu denti ajuta sana baada  ya  kufanyishwa ngo...
  • PICHA 5:MSANII WA BONGO FLEVA LIVE ANASWA AKINUNUA MACHANGUDOA
    WAKATI wasanii wakitakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuenzi maadili mema kwa jamii ya Kitanzania, mambo yamekuwa kinyume, baada ya nyota...
  • BARUA NZITO KWA DIAMOND PLATNUM HII HAPA
                                                   KWAKO Nasibu Abdul ‘Diamond’. Bila shaka u-mzima wa afya na unaendelea na michakato y...
  • LAANA HII: PICHA ZA UCHI ZA MWANAFUNZI MATILDA WA MUMESCO ARUSHA ZAVUJA...
    Mwanadada huyu( Matilda Singano ) amekuwa akiwatumia wanaume picha hizo kwa ajili ya kuwatega.Embu tizama mwenyewe picha hizi za mwanadada h...
  • KELELE ZA MIGUNO YA KIMAPENZI KUTOKA CHUMBA CHA JIRANI ZINANIPAGAWISHA
    Mimi ni Kijana wa Miaka 25, nimeanza kazi hivi karibuni ikanilazimu kutoka nyumbani na kupanga maeneo  ya  kijitonyama ...Sasa hi...
  • PICHA ZA UTUPU/UCHI ZA MAUNDA ZORO ZILIZOSAMBAA MITANDAONI: NI LAANA KWA KWELI
    Niwazi picha zenyewe zinajieleza hapa chini
  • KAMERA ZETU ZIMEMNASA MAMA HUYU WA KISHUA HUKO MASAKI DAR AKIWA AMEKAA VIBAYA.JINA LAKE HALIJATAMBULIKA
      PICHA NYINGINE ZIMEFICHWA HAPA
  • FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI (TENDO LA NDOA)
                                                          1 : Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo Wanawake ambao hufika kilele angalau...

LABELS

  • Maajabu
  • Mapenzi
  • Udaku
Copyright 2014 ULIMWENGU
Template By Ridwan Hex And Game Gratis